Saturday, 31 May 2014

MWANAMKE-MVUTIE MWANAMME WAKO BILA KUSHTUKIWA

 Kubadili mtindo wa kujikwatua.
Mwanamke anaweza kuwa amezoea
kujikwatua kwa namna fulani lakini
baada ya muda akaamua kubadili
muonekanao wake kwa kubadilisha aina
mpya ya kujikwatua kwa kuongeza
vikorombwezo fulani fulani akitegemea
mwenzi wake ata notes lakini asijue
kwamba wanaume kwenye jambo hilo
wala haliwagusi kabisa mpaka wafanye
kushtuliwa.
Kwa hiyo nawashauri tu msije mkaumia
bure pale mnapoona wenzi wenu hawa
notice mabadiliko mliyoyafanya ndivyo
tulivyo....
2. Kubadili mtindo wa nywele.
Kwa kawaida wanawake hutumia muda
wao mwingi kutengeneza nywele zao ili
kujipa mwonekano mpya na pia
wakitarajia kwamba wenzi wao
watapenda, lakini cha kushangaza wenzi
wao wala haiwagusi na wala hawa notice
mabadiliko hayo ya nywele mpaka
wafanye kushtuliwa na wenzi wao. jambo
hilo huwa linawakwaza sana wanawake,
lakini labda tu niwape ushauri wa bure,
msiweke matarajio makubwa ya kudhani
kwamba mabadiliko ya nywele
mnayoyafanya yatawavutia wenzi wenu,
si kweli utafadhaika bure bora tu
mfanye kwa utashi wenu
3. Kubadili rangi za kucha
Wanaume wengi hawajui tofauti ya
rangi, kwa hiyo hata mwanamke abadili
rangi yake ya kucha kwa ajili ya ku
match na mavazi fulani aliyonunuliwa na
mwenzi wake au hata aliyonunua
mwenyewe anaweza kushangaa mwenzi
wake asishtukie jambo hilo. Ajabu eh!
4. Mkoba mpya.
Unaweza kukuta mwanamke kajinasibu
na kununua mkoba mpya wa gharama
baada ya kujinyima sana akitegemea
mwenzi wake atauona na kumsifia lakini
atashangaa mwenzi wake wala haulizi
anaona tu kama ni mkoba wa kawaida.
Lakini pia hata kama mkoba wenyewe
ume match na mavazi bado ni ngumu
kwa mwanaume ku notice na ndiyo
maana inawauma sana wanawake wengi.
Mtuhurumie tu, ndivyo tulivyo....
5. Kiatu kipya
Viatu navyo ni eneo lingine ambalo
wanaume hawa notice kabisa, mwanamke
anaweza kununua kiatu kipya akitarajia
mwenzi wake atakiona na kumsifia lakini
wala, labda tu kama mwanaume huyo
anapenda aina hiyo ya kiatu na aliwahi
kukisifia baada ya kumuona mwanamke
mwingine amekivaa na kikampendeza,
lakini kama si mpenzi wa viatu wala
mwanamke asitarajie kusifiwa, ni mpaka
pale atakapomshtua mwenzi wake kwa
kumuuliza kama kiatu alichovaa
kimempendeza au la na sije akashangaa
akijibiwa kwa kifupi tu, "ndiyo" bila
comments.
Kwa kawaida wanawake wanapenda
ukiwasifia kuhusu jambo fulani utoe na
comments japo kidogo tena kwa undani
kabisa....
6. Lebasi za ulimbwende na
makochokocho mengine
Hereni, bangili na kishaufu au kipini cha
puani kinaweza kumpa mwanamke
muonekano mpya, lakini muonekano huo
hauwezi kumshangaza mwanaume kama
mwanamke anavyotarajia, jambo hilo
huwa linawakera sana wanawake lakini
ukweli ndiyo huo wanaume
hawasumbuliwi na vitu vidogo vidogo.
7. Pambo jipya chumbani au
kitandani
Mwanamke anaweza kubadili mwonekano
wa nyumba au wa chumba cha kulala
akidhani kwamba jambo hilo litamvutia
mwenzi wake. si kweli wanaume hawako
hivyo anaweza akafika nyumbani na
kuona kama vile hakuna kilichofanyika
mpaka afanye kushtuliwa na mwenzi
wake kwa kuulizwa kama ameionaje
nyumba au chumba chao cha kulala.
haishangazi mwanaume akiuliza kwani
kuna nini....!
Kwa mwanamke jibu hili anaweza hata
kutamani kumtwanga mwanaume na
flower verse kwa hasira, lakini
mianaume ndivyo tulivyo, mtuhurumie
tu.

No comments:

Post a Comment